• HABARI MPYA

  Monday, May 23, 2011

  Wamisri kuchezesha Simba v Wydad  SHIRIKISHO la Soka wa Afrika (CAF) limeteua waamuzi kutoka Misri kuchezesha mechi ya mkondo mmoja kati ya Simba ya Tanzania na Wydad Casablanca ya Morocco, itakayofanyika Mei 28 mwaka huu Uwanja wa Petrosport mijini Cairo, Misri.
  Boniface Wambura, Ofisa Habari TFF amesema leo kwamba mechi hiyo ya kutafuta timu ya kucheza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika itaanza saa 12 kamili jioni kwa saa za Cairo.
  Waamuzi hao ni Farouk Mohamed atakayepuliza filimbi wakati wasaidizi wake ni Mohamed Waleed na Hassan Sherif. Mwamuzi wa mezani (fourth official) ni Omar Fahim wakati Kamishna wa mchezo huo ni Magdy Shams El Din kutoka Sudan.
  Mshindi atacheza kundi B pamoja na timu za Al Ahly ya Misri, Esperance ya Tunisia na Moloudia Club d’Alger ya Algeria. Timu itakayoshindwa itaingia katika hatua ya 16 bora ya michuano ya Kombe la Shirikisho ambapo itacheza mechi ya kwanza nyumbani dhidi ya Daring Club Motema Pembe ya DRC kati ya Juni 10, 11 na 12 mwaka huu.
  Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Muhsin Balhabou ndiye atakayeongoza msafara wa timu ya Simba kwenda Cairo kwa ajili ya mechi hiyo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: Wamisri kuchezesha Simba v Wydad Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top