• HABARI MPYA

  Saturday, July 09, 2016

  TAMBWE, MATHEO HATARINI KUWAKOSA MEDEAMA FC JUMAMOSI IJAYO TAIFA

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI Mrundi, Amissi Joselyn Tambwe hakufanya mazoezi Yanga leo kutokana na kusumbuliwa na Malaria, klabu yake ikijiandaa na mchezo wa Kundi A Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Medeama ya Ghana Jumamosi ijayo.
  Tambwe alikwenda hospitali leo kwa matibabu na anatarajiwa kurejea mazoezini Jumatatu, wakati mshambuliaji mwingine, Matheo Anthony alishindwa kumaliza mazoezi leo baada ya kuumia jioni.
  Tambwe aliukosa mchezo uliopita dhidi ya TP Mazembe kutokana na kuwa anatumikia adhabu ya kadi – na sasa anaweza kuikosa pia mechi ijayo na Medeama kwa sababu za afya.
  Amissi Tambwe ameshindwa kufanya mazoezi leo kutokana na kusumbuliwa na Malaria

  Yanga inaendelea na mazoezi Uwanja wa Boko Veterani, Dar es Salaam huku ikiwa imeweka kambi hoteli Ludger Plazza, Kunduchi kujiandaa na mchezo wa tatu wa kundi lake.
  Tayari Yanga SC itawakosa beki Mwinyi Hajji Mngwali, viungo Deus Kaseke na Geoffrey Mwashiuya katika mchezo huo kutokana na kuwa majeruhi.
  Kaseke aliumia kwenye ajali ya pili, wakati Mngwali na Mwashiuya wote wanasumbuliwa na maumivu ya goti na hawataweza kucheza mchezo huo Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Yanga inahitaji ushindi dhidi ya Medeama baada ya kupoteza mechi zote mbili za mwanzo wakifungwa 1-0 mara zote – na Mo Bejaia nchini Algeria Juni 19 na TP Mazembe ya DRC Dar es Salaam Juni 28.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TAMBWE, MATHEO HATARINI KUWAKOSA MEDEAMA FC JUMAMOSI IJAYO TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top