• HABARI MPYA

  Saturday, July 23, 2016

  ULIMWENGU AUMIA GOTI LUBUMBASHI, KUWAKOSA MO BEJAIA JUMATANO

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Thomas Emmanuel Ulimwengu ameumia goti la mguu wa kushoto ambalo litamuweka nje si chini ya wiki mbili tangu sasa.
  Uli, maarufu kama Rambo mjini Lubumbashi, yalipo maskani ya klabu yake, TP Mazembe ameumia leo akiichezea klabu yake hiyo katika mchezo wa kirafiki dhidi ya timu B.
  Mazembe ipo katika maandalizi ya mwisho ya mchezo wa kwanza wa mzunguko wa pili Kundi A Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya MO Bejaia ya Algeria- maana yake Ulimwengu ataukosa mchezo huo wa Jumatano Uwanja wa TP Mazembe mjini Lubumbashi.
  Mguu wa Thomas Ulimwengu katika picha ndogo iliyoambatanishwa namna ulivyoumia 
  “Nimeumia goti leo, tulikua na mechi ya kirafiki na timu yetu ndogo,”alisema Ulimwengu akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE kutoka Lubumbashi leo.
  Ulimwengu sasa atafanyiwa vipimo kesho ili kujua ameumia kiasi gani na atakuwa nje kwa muda gani- lakini taarifa za awali ni kwamba hatacheza Jumatano dhidi ya MO Bejaia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ULIMWENGU AUMIA GOTI LUBUMBASHI, KUWAKOSA MO BEJAIA JUMATANO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top