• HABARI MPYA

  Saturday, July 23, 2016

  WAARABU TENA KUCHEZESHA YANGA NA MEDEAMA JUMANNE

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MCHEZO wa marudiano Kundi A Kombe la Shirikisho Afrika kati ya wenyeji, Medeama ya Ghana na Yanga ya Dar es Salaam utachezeshwa na marefa wa Morocco.
  Hao ni Redouane Jiyed atakayepuliza filimbi akisaidiwa na Mohamed Lahmidi na Hicham Ait Abbou watakaoshika vibendera.
  Yanga SC imeondoka leo kwenda Ghana kwa ajili ya mchezo wa marudiano na wenyeji Medeama, Kundi A Kombe la Shirikisho Afrika, lakini beki Mtogo mwenye asili ya Ivory Coast, Vincent Bossou ameachwa Dar es Salaam.
  Bossou ambaye anatumikia adhabu ya kadi mbili za njano ni kati ya wachezaji watatu waliobaki Dar es Salaam, wengine wakiwa ni viungo Geoffrey Mwashiuya na Deus Kaseke ambao ni majeruhi.

  Lakini kocha Mholanzi, Hans van der Pluijm amesema pengo la Bossou litazibwa na Nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’ ambaye yuko fiti.
  “Tuna viungo wa kutosha, sifurahii kuwakosa Kaseke na Mwashiuya, lakini kwa kuwa hawapo kwa sababau ambazo zipo nje uya uwezo wetu, wengine watacheza badala yao,”aliema Pluijm juzi usiku kabla ya safariya Ghana.
  Yanga watakuwa wageni wa Medeama Jumanne ya Julai 26, mwaka huu Uwanja wa Sekondi Sports au Essipong mjini Sekondi-Takoradi, Ghana katika mchezo huo wa kwanza wa marudiano mzunguko wa pili Kombe la Shirikisho, na siku inayofuata vinara wa kundi hilo, TP Mazembe wataikaribisha Mouloudia Olympique Bejaia mjini Lubumbashi.
  Timu hizo zitarudiana kiasi cha wiki baada ya kutoa sare katika mechi zao za kwanza, Yanhga 1-1 na Medema ana MO Bejaia 0-0 na Mazembe.
  Mazembe inaongoza Kundi A kwa pointi zake saba, ikifuatiwa na MO Bejaia pointi tano, Medeama pointi mbili, wakati Yanga yenye pointi moja inashika mkia.  
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WAARABU TENA KUCHEZESHA YANGA NA MEDEAMA JUMANNE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top