• HABARI MPYA

    Wednesday, February 04, 2026

    FOUNTAIN GATE YAAMBULIA SARE 1-1 NA NAMUNGO FC BABATI


    TIMU ya Fountain Gate imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Namungo FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Babati mkoani Manyara.
    Kiungo Kassim Shaaban Haruna alianza kuifungia Fountain Gate dakika ya 44, kabla ya mshambuliaji Mkongo, Fabrice Ngoy Wa Ngoy kuisawazishia Namungo FC dakika ya 68.
    Kwa matokeo hayo, Fountain Gate inafikisha pointi 12 katika mchezo wa 12, ingawa wanabaki nafasi ya 12 — wakati Namungo FC inafikisha pointi 19 katika mchezo wa 11, ingawa nayo inabaki nafasi ya nne. 
    Next
    This is the most recent post.
    Older Post
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: FOUNTAIN GATE YAAMBULIA SARE 1-1 NA NAMUNGO FC BABATI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top