• HABARI MPYA

  Sunday, July 24, 2016

  AZAM FC WAIENDEA YANGA KAMBINI ZANZIBAR

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  AZAM FC inatarajiwa kuondoka kesho mjini Dar es Salaam kwenda visiwani Zanzibar kuweka kambi ya kujiandaa na msimu mpya kwa ujumla.
  Azam FC itamenyana na mabingwa wa mataji yote nchini msimu uliopita, Yanga SC Agosti 17 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa kufungua pazia la msimu mpya.
  Na baada ya ushindi wa mabao 5-0 jana dhidi ya Mshikamano FC ya Kinondoni, Azam inakwenda kujichimbia rasmi Zanzibar chini ya Kocha wake mpya, Zeben Hernandez Rodriguez kutoka Hispania kuanza maandalizi rasmi.

  Mchezo wa jana ulikuwa wa tatu wa kujipima ubavu chini ya Rodriguez, anayesaidiwa na Waspaniola wenzake watupu, ambaye alipata fursa ya kuwatathimini wachezaji wake wote wakiwemo wanaofanya majaribio.
  Mechi mbili za awali ambazo timu hiyo imeshinda ni zile dhidi ya Ashanti United iliyowachapa mabao 2-0 kabla ya kuwatandika Friends Rangers 2-1 Jumatano iliyopita.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC WAIENDEA YANGA KAMBINI ZANZIBAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top