• HABARI MPYA

    Thursday, July 21, 2016

    KOZI YA MAREFA WA FIFA NCHINI KUFANYIKA JULAI 24 DAR

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KOZI za Waamuzi wa Mpira wa Miguu wa Tanzania sasa itaanza Julai 25, 2016 badala ya Julai 24, 2016 kama ilivyotangazwa hapo awali.
    Kozi hiyo itaanza moja kwa moja kwa waamuzi wenye Beji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu la Kimataifa (FIFA) ambao kwa sasa idadi yao ni 18 na waaamuzi waandamizi ambao idadi yao ni 12.
    Itaanza kwa ratiba ya waamuzi wote kuchukuliwa vipimo (physical fitness test) kwa kila mwamuzi chini ya wawezeshaji wa kozi hiyo kutoka FIFA.
    Wawezeshaji hao ni Carlos Henrique kutoka Afrika Kusini, Mark Mzengo kutoka Malawi na Felix Tangawarima wa Zimbabwe. Waamuzi hao wenye Beji ya FIFA na wale wanaotarajiwa kuveshwa beji hiyo, wanatakiwa kuripoti Dar es Salaam Julai 24, 2016.

    Baada ya vipimo, darasa la waamuzi hao litaanza kwa nadharia na vitendo. Darasa hilo litafikia mwisho Julai 29, 2016 kabla ya kuanza darasa la waamuzi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), Ligi Daraja la Kwanza ya StarTimes (FDL) na Ligi Daraja la Pili (SDL) kwa msimu wa 2016/2017.
    Mara baada ya programu hiyo, kozi itaendelea kwa waamuzi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), Ligi Daraja la Kwanza ya StarTimes (FDL) na Ligi Daraja la Pili (SDL) na makamishna wa michezo kwa msimu wa 2016/2017 na kwamba wahusika wote watajigharamia gharama zote.
    Waamuzi hao wa ligi ya ndani wataripoti na kujisajili Kituo cha Dar es Salaam Julai 28, 2016 na na Julai 29, 2016 na Julai 30, watakuwa na kozi ya kitathmini kasi kwa kukimbia kabla ya Agosti 1 na 2, 2016 kuwa na semina darasani na mitihani wakati Agosti 3, 2016 kutakuwa na semina na mitihani kwa makamishna mbalimbali wa michezo ya mpira wa miguu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KOZI YA MAREFA WA FIFA NCHINI KUFANYIKA JULAI 24 DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top