• HABARI MPYA

  Tuesday, July 26, 2016

  PIGO ARSENAL, MARTESACKER NJE MIEZI MITANO

  MAANDALIZI ya Arsenal kuelekea msimu mpya yameingia doa, kufuatia beki tegemeo, Per Mertesacker kuumia goti na kuambiwa atakuwa nje ya Uwanja kwa miezi mitano.
  Beki huyo wa kati Mjerumani, ambaye anatarajiwa kupewa Unahodha wa timu, hajasafiri na timu katika ziara ya California kwa ajili ya mechi mbili za kirafiki za Arsenal dhidi ya timu za MLS All-Stars na Chivas baada ya kuumia mazoezini.
  Hakuwa na dalili za Mertesacker mwenye umri wa miaka 31 kuhitaji upasuaji, lakini kutokuwepo kwake kunamuachia maumivu ya kichwa kocha Mfaransa, Arsene Wenger kuelekea msimu mpya.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: PIGO ARSENAL, MARTESACKER NJE MIEZI MITANO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top