• HABARI MPYA

  Saturday, July 30, 2016

  KASEKE AANZA MAZOEZI YANGA SC IKIJIFUA JANGWANI MARA YA KWANZA CHINI YA MANJI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KIUNGO Deus David Kaseke jana amefanya mazoezi na Yanga baada ya kukosekana kwa wiki tatu kutokana na maumivu aliyopata baada ya ajali ya pikipiki.
  Kaseke alikosekana Yanga SC katika mechi zote dhidi ya Medeama ya Ghana Kundi A Kombe la Shirikisho Afrika, wakitoa sare ya 1-1 nyumbani Dar es Salaam na kufungwa 3-1 Ghana baada ya ajali ya pikipiki.
  Lakini sasa kiungo huyo amepona majeraha yake naa anajaribu kurejea kwa ajili ya mchezo ujao Agosti 13 dhidi ya Mouloudia Olympique Bejaia Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Kocha Hans van der Pluijm akizungumza na kiungo Deus Kaseke mazoezini jana Jangwani
  Wachezaji wa Yanga wakinywa maji wakati wa mapumziko mafupi jana
  Yanga jana ilifanya mazoezi kwenye Uwanja wake wa Kaunda, makao makuu ya klabu, Jangwani, Dar es Salaam baada ya muda mrefu na labda kwa mara ya kwanza kabisa, tangu Yussuf Manji awe Mwenyekiti.
  Na kocha Mholanzi Hans van der Pluijm alilazimika kushuka Jangwani baada ya jitihada za kupata uwanja wa kukodi kama ilivyo ada yao kugonga mwamba jana.
  Yanga ilirejea Dar es Salaam Alhamisi usiku ikitokea Ghana ambako Jumanne ilipigwa 3-1 Medeama katika mfululizo wa mechi za Kundi A Kombe la Shirikisho.
  Na hicho kilikuwa kipigo cha tatu katika mechi nne, baada ya awali kufungwa 1-0 mara mbili nyumbani na ugenini, dhidi ya MO Bejaia Algeria na TP Mazembe Dar es Salaam.
  Beki Mtogo mwenye asili ya Ivory Coast, Vincent Bossou akipasha jana 
  Hassan Kessy naye ameendelea na mazoezi ingawa hawezi kucheza mashindano haya
  TP Mazembe ndiyo wanaongoza kundi hilo kwa pointi zao 10 baada ya kushinda mechi tatu na sare moja, wakifuatiwa na Bejaia na Medeama ambao kila mmoja ana pointi tano wakati Yanga yenye pointi moja inashika mkia. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KASEKE AANZA MAZOEZI YANGA SC IKIJIFUA JANGWANI MARA YA KWANZA CHINI YA MANJI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top