TIMU ya Mtibwa Sugar imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
Mabao ya Mtibwa Sugar yamefungwa na Fredrick Magata dakika ya 38 kwa penalti na Ismail Mhesa dakika ya 87, wakati la Tanzania Prisons limefungwa na George Mpole kwa penalti pia dakika ya nane.
Kwa ushindi huo, Mtibwa Sugar wanafikisha pointi 20 katika mchezo wa 12 na kusogea nafasi ya tatu kutoka ya tano, wakati Tanzania Prisons inabaki na pointi zake nane za mechi 10 sasa nafasi ya 15 kwenye ligi ya timu 16.



.png)
0 comments:
Post a Comment