• HABARI MPYA

    Sunday, February 08, 2026

    YANGA SC YACHAPWA 1-0 NA AS FAR RABAT NCHINI MOROCCO


    MATUMAINI ya Yanga SC kwenda Robo Fainali yameingia doa baada ya kuchapwa bao 1-0 na wenyeji, AS FAR Rabat katika mchezo wao wa Kundi B Ligi ya Mabingwa Afrika usiku huu Uwanja wa Olimpiki Jijini Rabat nchini Morocco.
    Bao lililoizamisha Yanga leo limefungwa na kiungo wa ulinzi, Anas Bach dakika ya 85.
    Mchezo mwingine wa Kundi B leo Al Ahly imejihakikishia kufuzu Robo Fainali baada ya sare ya 0-0 na wenyeji, JS Kabylie Uwanja wa Hocine Aït Ahmed mjini Tizi Ouzou nchini Algeria.
    Ahly wanafikisha pointi tisa ambazo zinaweza kufikiwa na AS FAR Rabat pekee, ambao sasa wana pointi nane, wakifuatiwa na Yanga pointi tano na JS Kabylie yenye pointi mbili baada ya timu zote kucheza mechi tano.
    Mechi za mwisho zitachezwa Februari 15, Yanga wakimalizia nyumbani na JS Kabylie na AS FAR Rabat wakimalizia ugenini na Al Ahly Uwanja wa Cairo International, Cairo.
    Next
    This is the most recent post.
    Older Post
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA SC YACHAPWA 1-0 NA AS FAR RABAT NCHINI MOROCCO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top