• HABARI MPYA

  Tuesday, July 26, 2016

  SIMBA YAUA 6-0 KIRAFIKI MORO, HAJIB NA BLAGNON KILA MMOJA MAWILI

  MABINGWA wa zamani nchini, Simba SC wameanza kuonjesha makali yao ya msimu mpya baada ya jioni ya leo kuwafunga mabao 6-0 Polisi Moro katika mchezo wa kirafiki uliofanyika Uwanja wa Highlands, Bigwa mkoani Morogoro.
  Simba iliyoweka kambi Chuo cha Biblia mjini humo kujiandaa na msimu mpya, ilionyesha kwamba msimu ujao itashindania mataji nchini kutokana na aina ya wachezaji iliyosajili kucheza vizuri.
  Mshambuliaji kutoka Ivory Coast, Frederick Blagnon alifunga mabao mawili sawa na Ibrahim Hajib, wakati mengine yalifungwa na Abdi Banda na Mohammed Mussa kila mmoja moja.
  Ibrahim Hajib (kushoto) amefunga mabao mawili leo

  Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Vincent Angban, Janvier Besala Bokungu/Hamad Juma dk46, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’/Abdi Banda dk59, Method Mwanjali, Novat Lufunga/Juuko Murushid dk46, Muzamil Yassin, Mohammed ‘Mo’ Ibrahim/Said Ndemla dk46, Shizza Kichuya/Mohammed Mussa dk70, Frederick Blagnon/Mussa Mgosi dk25/Peter Mwalyanzi dk70, Ibrahim Hajib/Awadh Juma dk75 na Jamal Mnyate/Danny Lyanga dk46.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA YAUA 6-0 KIRAFIKI MORO, HAJIB NA BLAGNON KILA MMOJA MAWILI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top