• HABARI MPYA

  Sunday, July 24, 2016

  KOLO TOURE ATUA SCOTLAND KUMALIZIA SOKA YAKE CELTIC

  Beki mkongwe, Kolo Toure akiwa amepozi na jezi ya Celtic baada ya kusaini Mkataba wa mwaka mmoja PICHA ZAIDI GONGA HAPA 

  TAKWIMU ZA TOURE KATIKA LIGI 2015/16 

  Mechi alizocheza: 14
  Mabao aliyofunga: 1
  Mashuti sahihi: asilimia 100
  Nafasi alizotengeneza: 1
  Pasi sahihi: Asilimia 81
  Duels won: Asiliami 55
  Kadi za njano/nyekundu: 1/0
  KLABU ya Celtic ya Scotaldn imekamilisha uhamisho wa beki wa kimataifa wa Ivory Coast, Kolo Toure kutoka Liverpool ya England.
  Beki huyo wa zamani wa Arsenal, anakwenda kuungana tena na kocha wake aliyekuwa naye Liverpool, Brendan Rodgers.
  Toure, mwenye umri wa miaka 35, anajiunga na Celtic kwa Mkataba wa mwaka mmoja kwa mujibu wa taarifa ya mabingwa hao wa Scotland.
  "Nimekuja kujiunga na moja ya klabu duniani na kipaumbele kwangu kuwa hapa,"alisema.
  Rodgers alimsajili Toure Liverpool mwaka 2013, baada ya awali kuzichezea Manchester City na Arsenal.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KOLO TOURE ATUA SCOTLAND KUMALIZIA SOKA YAKE CELTIC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top