• HABARI MPYA

  Saturday, July 30, 2016

  SIMBA YA OMOG YAENDELEZA WIMBI LA USHINI DHIDI YA ‘VITIMU’ VYA MORO

  MABINGWA wa zamani nchini, Simba SC wameendeleza wimbi la ushindi katika mechi za kujipima ngugvu baada ya jana kuifunga Moro Kids mabao 2-0 Uwanja wa Highlands, Bigwa mkoani Morogoro.
  Huo unakuwa ushindi wa pili kwa Simba iliyoweka kambi kayika Chuo cha Biblia mjini hapa kujiandaa na msimu mpya, baada ya Jumanne kuifunga mabao 6-0 Polisi Morogoro kwenye Uwanja huo huo.
  Mabao ya Simba iliyo chini ya kocha mpya, Mcameroon Joseph Marius Omog katika mchezo wa jana dhiid ya Moro Kids yalifungwa na washambuliaji Ibrahim Hajib na Danny Lyanga.
  Kwa Hajib (pichani kushoto) jana alirudia kufunga baada ya Jumanne pia kufunga mara mbili katika ushindi wa 6-0, mabao mengine yakifungwa na mshambuliaji kutoka Ivory Coast, Frederick Blagnon mawili pia, Abdi Banda moja sawa na Mohammed Mussa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA YA OMOG YAENDELEZA WIMBI LA USHINI DHIDI YA ‘VITIMU’ VYA MORO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top