• HABARI MPYA

  Thursday, July 28, 2016

  ZAMALEK YAFUKUZA KOCHA ILIYEMUAJIRI MEI TU

  KOCHA Mohamed Helmi amejiuzulu Zamalek usiku wa jana kufuatia kipigo cha pili ndani ya siku 10 cha timu hiyo kutoka kwa Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, amesema Mwenyekiti wa klabu, Mortada Mansour.
  Bao la kujifunga la dakika za lalama la Ali Gabr lilitosha kuifanya Zamalek ipoteze mchezo mwingine wa Ligi ya Mabingwa kwa Sundowns, safari hii mjini Pretoria wenyejji wakifuzu Nusu Fainali huku wana mechi moja mkononi.
  Pamoja na kufungwa, Zamalek bado wana nafasi ya kwenda Nusu Fainali iwapo wataepuka kufungwa nyumbani na Enyimba ya Nigeria katika mchezo wao wa mwisho wa Kundi B.
  Kocha Mohamed Helmi amejiuzulu Zamalek baada ya kipigo cha Mamelodi jana
  Pamoja na hayo, Mansour, ambaye inafahamika ni mtu wa maamuzi ya haraka ya ghadhabu alijibu haraka kukubali kujiuzulu kwa Helmi, aliyeichukua klabu hiyo Mei mwaka huu baada ya kufukuzwa kwa Mscotland, Alex McLeish.
  "Mbadala wa Helmi atakuwa mgeni. Tutachagua kati ya Muargentina Enzo Trossero na Mbelgiji Georges Leekens,” alisema Mwanasheria huyo mtata katika mahojiano ya Televisheni baada ya mechi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ZAMALEK YAFUKUZA KOCHA ILIYEMUAJIRI MEI TU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top