• HABARI MPYA

    Wednesday, July 27, 2016

    HIGUAIN ATUA KWA DAU LA REKODI JUVE KUTOKA NAPOLI

    Gonzalo Higuain amejiunga na Juventus kwa ada ya uhamisho ya Pauni Milioni 76 kutoka Napoli  PICHA ZAIDI GONGA HAPA 


    USAJILI GHALI ZAIDI KUWAHI KUTOKEA

    Pauni Milioni 86 Gareth Bale - 2013 (Kutoka Tottenham kwenda Real Madrid) 
    Puni Milioni 80 Cristiano Ronaldo - 2009 (Kutoka Manchester United kwenda Real Madrid) 
    Pauni Milioni 71.5 Neymar - 2013 (Kutoka Santos kwenda Barcelona)
    Pauni Milioni 65 Luis Suarez - 2014 (Kutoka Liverpool kwenda Barcelona)
    Pauni Milioni 63 James Rodriguez - 2014 (Kutoka Monaco kwenda Real Madrid) 
    KLABU ya Juventus imemsajili mshambuliaji Gonzalo Higuain kwa mkataba wa miaka mitano kwa ada ya uhamisho ya Pauni Milioni 76 kutoka Napoli, zote za Italia.
    Ada ya uhamisho italipwa kwa awamu mbili, na mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina mwenye umrin wa miaka 28 atalipwa mshahara wa Pauni Milioni 6.3 kwa mwaka baada ya kodi.
    Taarifa ya Juventus imesema; "Juventus Football Club leo inaweza kuthibitisha imemsajili Gonzalo Higuain kwa dau la Euro Milioni 90, zitakazolipwa kwa awamu mbili ndani ya miaka miwili. Mchezaji huyo amesaini Mkataba wa miata mitano,". Na kwa usajili huo, Higuain anaingia kwenye orodha ya wachezaji ghali kuwahi kusajiliwa duniani.
    Orodha hiyo inaongozwa na Gareth Bale aaliyesajiliwa kwa Pauni Milioni 86 mwaka 2013 kutoka Tottenham kwenda Real Madrid, akifuatiwa na Cristiano Ronaldo aliyesajiliwa kwa Puni Milioni 80 mwaka 2009 kutoka Manchester United kwenda Real Madrid. 
    Wengine ni Neymar aliyesajiliwa kwa Pauni Milioni 71.5 mwaka 2013 kutoka Santos kwenda Barcelona, Luis Suarez aliyesajiliwa kwa Pauni Milioni 65 mwaka 2014 kutoka Liverpool kwenda Barcelona na James Rodriguez aliyesajiliwa kwa Pauni Milioni 63 mwaka 2014 kutoka Monaco kwenda Real Madrid.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: HIGUAIN ATUA KWA DAU LA REKODI JUVE KUTOKA NAPOLI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top