• HABARI MPYA

  Thursday, July 28, 2016

  SIMBA KUMENYANA NA INTECLUBE YA ANGOLA AGOSTI 8 TAIFA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  SIMBA SC itamenyana na Interclube ya Angola Agosti 8, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo maalum wa tamasha la klabu hiyo, maarufu kama Simba Day.
  Interclube wanatarajiwa kuwasili nchini Agosti 6 kabla ya mchezo huo maalum utakaotumika kutambulisha kikosi kipya cha Wekundu wa Msimbazi na benchi la Ufundi.
  Kwa sasa, Simba imeweka kambi Chuo cha Biblia eneo la Bigwa mkoani Morogoro chini ya kocha wake Mkuu, Mcameroon, Joseph Marius Omog kujiandaa na msimu mpya.
  Baadhi ya wachezaji waliopo kambini Morogoro beki Janvier Besala Bokungu, viungo Mussa Ndusha, Sanga Bahende na mshambuliaji Cedrick Masanga wote kutoka DRC.
  Wengine ni washambuliaji Frederick Blagnon kutoka Ivory Coast na Ndjack Anong Guy Serges kutoka Cameroon, Moses Chibandu, Said Mussa, Kelvin Falu, Vincent Costa wote wapya pamoja na wa zamani Nahodha Mussa Hassan Mgosi, Juuko Murshid, Vincent Angban, Awadh Juma, Said Ndemla, Peter Mwalyanzi, Peter Manyika, Dennis Richard, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Hijja Ugando, Novatus Lufunga, Mwinyi Kazimoto, Danny Lyanga na Ibrahim Hajib.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA KUMENYANA NA INTECLUBE YA ANGOLA AGOSTI 8 TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top