• HABARI MPYA

    Tuesday, July 26, 2016

    AZAM FC YAMALIZANA NA STRAIKA HATARI LA MEDEAMA, KAZI NZURI YA SAAD KAWEMBA

    Na Mwandishi Wetu, SEKONDI
    AZAM FC imefikia makubaliano na klabu ya Medeama FC ya Ghana juu ya kumsajili mshambuliaji, Enoch Atta Agyei.
    Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba yupo Ghana kwa ajili ya kukamilisha usajili wa mchezaji huyo na taarifa zinasema ametekeleza jukumu hilo vizuri.
    Mshambuliaji huyo wa zamani wa Windy Professionals aliivutia Azam FC akiichezea Medeama wiki tatu zilizopita Dar es Salaam katika mchezo wa Kundi A Kombe la Shirikisho.
    Na tangu hapo, Azam FC ikaanza harakati za kuipata saini yake kabla ya jana kukamilisha mpango huo Uwanka wa Essipong Sports mjini Sekondi. 
    Enock Atta Agyei (kulia) akipambana na Simon Msuva wa Yanga
    Kinda huyo wa miaka 17, alifunga mabao 17 katika Ligi Daraja la Kwanza ya GN Bank akiwa na Windy Professionals kabla ya kuhamia Medeama SC .
    Yanga walishituka kumuona Kawemba katika mazoezi yao Uwanja wa Essipong Sports mjini Sekondi jioni ya jana, wakidhani amekwenda kuwahujumu, kumbe kafuata mchezaji.  
    Mtu anayedaiwa kuwa Ni Saad kawemba (katikati) akizungumza na Mghana leo Uwanja wa Essipong Sports
    Mtu anayedaiwa kuwa ni Kawemba akiwa ametulia kwenye kiti na mwenyeji wake wa Ghana leo Uwanja wa Essipong, wakati Yanga na Medeama zikifanya mazoezi

    Hata hivyo, kwa mujibu wa habari za ndani kutoka Azam FC, ambazo BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE imezipata ni kwamba Kawemba amekwenda huko kushughulikia mpango wa Azam TV kuonyesha moja kwa moja mechi hiyo kesho.

    "Kawemba amekwenda kwa ajili ya mambo ya Azam TV, na ameagizwa yeye kwa sababu anafahamiana na viongozi wengi wa mpira, si unajua yule alikuwa TFF,"kimesema chanzo.   
    Yanga ambayo jana ilifanya mazoezi kwenye Uwanja wa shule ya Bohar mjini hapa, siku moja baada ya kuwasili hapa, usiku wa Jumamosi kutoka Dar es Salaam imepania kushinda kesho ili kufufua matumaini ya kwenda Nusu Fainali.
    Mchezo Hao utachezeshwa naRedouane Jiyed atakayepuliza filimbi akisaidiwa na Mohamed Lahmidi na Hicham Ait Abbou watakaoshika vibendera.
    TP Mazembe wataikaribisha Mouloudia Olympique Bejaia ya Algeria Juamatno mjini Lubumbashi katika mchezo mwingine wa kundi hilo.
    Timu hizo zitarudiana kiasi cha wiki baada ya kutoa sare katika mechi zao za kwanza, Yanhga 1-1 na Medema ana MO Bejaia 0-0 na Mazembe.
    Mazembe inaongoza Kundi A kwa pointi zake saba, ikifuatiwa na MO Bejaia pointi tano, Medeama pointi mbili, wakati Yanga yenye pointi moja inashika mkia.  
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM FC YAMALIZANA NA STRAIKA HATARI LA MEDEAMA, KAZI NZURI YA SAAD KAWEMBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top