• HABARI MPYA

  Saturday, July 30, 2016

  MKWASA ASITISHA KAMBI TAIFA STARS BAADA YA KLABU KUOMBA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KUTOKANA na maombi ya klabu nyingi za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kutaka kuandaa wachezaji kwa ajili ya msimu mpya unaotarajiwa kuanza wiki tatu zijazo, Kocha Mkuu wa Tanzania, Charles Boniface Mkwasa ameahirisha kambi iliyokuwa ianze Jumatatu Agosti mosi, mwaka huu.
  Wachezaji ambao Mkwasa amewaita wanatoka kwenye klabu mbalimbali na ambazo zinaongoza kutoa nyota wengi ni Simba SC, Young Africans SC, Azam FC na Mtibwa Sugar FC sasa watabaki na klabu zao.
  Hivyo basi, Mkwasa sasa atakuwa anafuatilia mwenendo wa nyota 24 aliowaita kwenye michezo mbalimbali ya kirafiki wa klabu hizo inayofanyika kabla ya kuanza Ligi Kuu Tanzania Bara (Pre-season matches) na michezo ya raundi ya kwanza na pili ya Ligi Kuu kabla ya kukiita tena kikosi hicho kwa ajili ya safari ya kwenda Nigeria.
  Charles Boniface Mkwasa ameita chipukizi kibao kuunda Taifa Stars
  Taifa Stars ina mchezo na jijini Lagos, Nigeria Septemba 2, 2016 ambao ni wa kukamilisha ratiba katika kundi G baada ya Misri kusonga mbele wakati Chad kujitoa.
  Wachezaji walioitwa ni Makipa; Deogratius Munishi (Yanga), Aishi Manula (Azam) na Benny Kakolanya (Prisons), mabeki; Kelvin Yondani (Yanga), Aggrey Morris (Azam), Oscar Joshua (Yanga), Mohamed Husein ‘Tshabalala’ (Simba), Juma Abdul (Yanga) na Erasto Nyoni (Azam).
  Viungo: Himid Mao, Mohamed Ibrahim, Shiza Kichuya, Jonas Mkude, Ibrahim Jeba, Mwinyi Kazimoto, Farid Mussa, Juma Mahadhi na Hassan Kabunda, wakati washambuliaji ni Simon Msuva, Joseph Mahundi, Jamal Mnyate, Ibrahim Ajib, John Bocco na Jeremia Juma.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MKWASA ASITISHA KAMBI TAIFA STARS BAADA YA KLABU KUOMBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top