• HABARI MPYA

    Saturday, July 09, 2016

    SHIZZA NA WENGINE 29 WAENDA KAMBINI SIMBA SC MAANDALIZI YA MSIMU MPYA

    Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
    KIUNGO mpya wa Simba, Shizza Ramadhani Kichuya ni miongoni mwa wachezaji wanaotarajiwa kuingia kambini Morogoro, Simba SC ikianza rasmi maandalizi ya msimu mpya.
    Shizza ni kati ya wachezaji watatu wapya wa Simba waliosajiliwa kutoka Mtibwa Sugar, wengine wakiwa ni Muzamil Yassin na Mohamed ‘Mo’ Ibrahim.
    Rais wa Simba SC, Evans Elieza Aveva ameiambia BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE leo kwamba wachezaji 30 wataingia kambini kesho, ingawa hakuwataja majina.
    Shizza Kichuya (kushoto) akimlamba chenga Jonas Mkude wakati Simba ilipokutana na Mtibwa Sugar msimu uliopita
    Lakini BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE inafahamu ni wachezaji 25 tu hadi leo walikuwa tayari mjini Dar es Salaam na wengine walikuwepo kwenye kambi ya awali ya mazoezi Chuo cha Polisi, Kurasini mjini Dar es Salaam. 
    Hao ni pamoja na Nahodha Mussa Hassan Mgosi, Vincent Angban, Awadh Juma, Said Ndemla, Peter Mwalyanzi, Peter Manyika, Dennis Richard, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Hijja Ugando, Novatus Lufunga, Mwinyi Kazimoto, Danny Lyanga na Ibrahim Hajib kwa upande ambao walikuwa na timu hadi msimu uliopita. 
    Shizza Kichuya amejiunga na Simba SC kutoka Mtibwa Sugar ya Morogoro

    Wapya waliokuwa wameripoti hadi jana mjini Dar es Salaam ni Shizza Kichuya, Mohammed Kijiko, Moses Chibandu, Said Mussa, Muzamil Yassin, Mohammed ‘Mo’ Ibrahim, Frederick Blagnon, Kelvin Falu, Vincent Costa, Method Mwanjali, Janvier Besala Bokungu na Mussa Ndusha. 
    Kocha Mcameroon Joseph Marius Omog na Msaidizi wake, Mganda Joseph Marius Omog wanatarajiwa kupanda basi na wachezaji hao 30 mapema leo kwa safari ya Morogoro.
    Wachezaji wengine ambao inadaiwa wamefikia makubaliano na uongozi wa Simba ni pamoja na mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi, Laudit Mavugo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SHIZZA NA WENGINE 29 WAENDA KAMBINI SIMBA SC MAANDALIZI YA MSIMU MPYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top