• HABARI MPYA

    Tuesday, July 26, 2016

    MKWASA ATAJA TAIFA STARS YA CHIPUKIZI KIBAO

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KOCHA Mkuu timu ya Mpira Tanzania ‘Taifa Stars’, Charles Boniface Mkwasa ameita kikosi cha wachezaji 24 watakaoanza kambi ya awali kuajindaa na mchezo dhidi ya Nigeria utakaofanyika Lagos, Septemba 2, 2016.
    Kwa mujibu wa Mkwasa, timu hiyo itaingia kambini Agosti 1, 2016 na itadumu kwa siku tano tu kabla ya kuvunjwa na kuitwa tena mwishoni mwa mwezi Agosti, 2016 kujiandaa na kambi ya mwisho na moja kwa moja itakuwa ni kwa ajili ya safari kwenda Nigeria.
    Katika kikosi hicho, Mkwasa hajawaita Nahodha, Mbwana Samatta wa KRC Genk ya Ubelgiji na Thomas Ulimwengu wa TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kwa sababu ya majukumu waliyonayo kwenye klabu zao kwa sasa.
    Charles Boniface Mkwasa ameita chipukizi kibao kuunda Taifa Stars
    Kadhalika, nyota hao wataungana na wenzao nchini Nigeria kwa kuwa mchezo huo upo kwenye kalenda ya CAF na ni wa mashindano. Mchezo huO ambao ni wa kukamilisha ratiba, Mkwasa amesema utakuwa mgumu kwani Nigeria wamebadili benchi la ufundi hivyo kila timu inaungalia mchezo huu kwa jicho la pekee.
    Wachezaji walioitwa ni Makipa; Deogratius Munishi (Yanga), Aishi Manula (Azam) na Benny Kakolanya (Prisons), mabeki; Kelvin Yondani (Yanga), Aggrey Morris (Azam), Oscar Joshua (Yanga), Mohamed Husein ‘Tshabalala’ (Simba), Juma Abdul (Yanga) na Erasto Nyoni (Azam).
    Viungo: Himid Mao, Mohamed Ibrahim, Shiza Kichuya, Jonas Mkude, Ibrahim Jeba, Mwinyi Kazimoto, Farid Mussa, Juma Mahadhi na Hassan Kabunda, wakati washambuliaji ni Simon Msuva, Joseph Mahundi, Jamal Mnyate, Ibrahim Ajib, John Bocco na Jeremia Juma.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MKWASA ATAJA TAIFA STARS YA CHIPUKIZI KIBAO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top