• HABARI MPYA

  Friday, July 29, 2016

  SIMBA ‘YAMNYAKUA’ MWADINI ALI WA AZAM FC

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  SIMBA SC imefanikiwa kuwapata wachezaji wawili wa mkopo kutoka Azam FC, kipa Mwadini Ali na mshambuliaji Ame Ali ‘Zungu’.
  Wazanzibari hao wanatarajiwa kuripoti kambini Jumatatu mjini Morogoro kuelekea mchezo wa Simba Day Agosti 8, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  “Mwadini na Ame wote tumewapata kwa mkopo wa muda mrefu wa msimu,”kimesema chanzo jana. 
  Wiki iliyopita Simba ilileta wachezaji wawili kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), kiungo Sanga Bahende na mshambuliaji Cedrick Masanga, wote kutoka FC Lupopo ya Lubumbashi.
  Mwadini Ali atajiunga na Simba SC Jumatatu mjini Morogoro

  Wakongo hao walifanya idadi ya wachezaji wa kigeni waliokuja kwa majaribio Simba kufika saba, baada ya mabeki Mzimbabwe, Method Mwanjali, Janvier Besala Bokungu, kiungo Mussa Ndusha wote kutoka DRC, washambuliaji Frederick Blagnon kutoka Ivory Coast na Ndjack Anong Guy Serges kutoka Cameroon.
  Simba SC imeweka kambi mjini Morogoro kujiandaa na msimu mpya na mbali na wachezaji hao wa kigeni, kuna wapya wengine ambao ni pamoja na watatu waliosajiliwa kutoka Mtibwa Sugar ya Morogoro, wote viungo Muzamil Yassin, Mohamed ‘Mo’ Ibrahim na Shizza Kichuya na Jamal Mnyate kutoka Mwadui FC. 
  Wengine ni Moses Chibandu, Said Mussa, Kelvin Falu, Vincent Costa wote wapya pamoja na wa zamani Nahodha Mussa Hassan Mgosi, Juuko Murshid, Vincent Angban, Awadh Juma, Said Ndemla, Peter Mwalyanzi, Peter Manyika, Dennis Richard, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Hijja Ugando, Novatus Lufunga, Mwinyi Kazimoto, Danny Lyanga na Ibrahim Hajib.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA ‘YAMNYAKUA’ MWADINI ALI WA AZAM FC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top