• HABARI MPYA

  Saturday, July 23, 2016

  MUDATHIR AFUNGA MBILI, AZAM FC YAITANDIKA KMC 5-0 KIRAFIKI CHAMAZI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  AZAM FC imeendeleza wimbi la ushindi katika mechi zake za kujipima nguvu chini ya makocha wapya kutoka kutoka Hispania, baada ya asubuhi ya leo kuifunga timu ya Halmashauri ya Kinondoni (KMC) mabao 5-0 Uwanja wa Azam Complex, Azam Dar e s Salaam.
  Shukrani kwao, wafungaji wa mabao hayo, Nahodha John Raphael Bocco, kiungo Mudathir Yahya Abbas mawili, Shaaban Iddi na Farid Mussa.
  Bocco alianza kufunga dakika ya tatu akimalizia kwa shuti kali pasi ya Shaaban Idd, kabla ya Mudathir Yahya kufunga la pili dakika ya sita akimalizia pasi ya Fuadi Ndayisenga aliye kwenye majaribio Azam FC.
  Mudathir akawainua tena vitini mashabiki wa Azam kufung bao la tatu dakika ya 14 kwa shuti kali akimalizia pasi ya Salum Abubakar ‘Sure Boy’ na Shaaban Idd akaipatia bao la nne Azam FC akitumia vema pasi ya Bocco. 
  Zikiwa zimesalia dakika mbili mchezo kumalizika, Mudathir Yanga akawafungia tena Mabingwa hao wa Afrika Mashariki na Kati bao la tano.
  Kikosi cha Azam kilichoanza kipindi cha kwanza; Aishi Manula, Erasto Nyoni, Bruce Kangwa, Aggrey Morris, Himid Mao ‘Ninja’, Jean Mugiraneza ‘Migi’, Mudathir Yahya, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, John Bocco ‘Adebayor, Shaaban Idd, Fuadi Ndayisenga.
  Kipindi cha pili; Metacha Mnata, Ismail Gambo ‘Kusi’, Gadiel Michael, Abdallah Kheri, David Mwantika, Abdallah Masoud ‘Cabaye’, Omary Wayne, Frank Domayo (C), Ramadhan Singano ‘Messi’/Farid Mussa, Rajab Odasi, Khamis Mcha ‘Vialli’
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MUDATHIR AFUNGA MBILI, AZAM FC YAITANDIKA KMC 5-0 KIRAFIKI CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top