• HABARI MPYA

    Monday, February 02, 2026

    VALENTINO AWEKA MBILI JKT TANZANIA YAICHAPA PAMBA 3-0 MBWENI


    WENYEJI, JKT Tanzania wameiadhibu Pamba Jiji FC kwa kuitandika mabao 3-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara ISIJI hui Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Mbweni, Dar es Salaam.
    Mabao ya JKT Tanzania yamefungwa na mshambuliaji Valentino Mashaka Kusengama mawili dakika ya 34 na 70 na winga Saleh Karabaka Kikuya dakika ya 55.
    Kwa ushindi huo, JKT Tanzania inafikisha pointi 24 katika mchezo wa 14 na kurejea kileleni mwa Ligi Kuu, wakati Pamba Jiji FC inabaki na pointi zake 17 za mechi 12 nafasi ya tano. 
    Next
    This is the most recent post.
    Older Post
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: VALENTINO AWEKA MBILI JKT TANZANIA YAICHAPA PAMBA 3-0 MBWENI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top