• HABARI MPYA

  Wednesday, July 27, 2016

  KALABA AIPELEKA MAZEMBE NUSU FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO

  BAO pekee la Mzambia Ranford Kalaba dakika ya 61, limeipa ushindi wa 1-0 TP Mazembe dhidi ya MO Bejaia ya Algeria katika mchezo wa Kundi A Kombe la Shirikisho Afrika jioni ya leo Uwanja wa Mazembe mjini Lubumbashi, DRC.
  Kwa ushindi huo, Mazembe inafikisha pointi 10 na kujihakikishia kwenda Nusu Fainali ikiwa inazizidi kwa pointi tano zote, Bejaia na Medeama ya Ghana zenye pointi tano kila moja kuelekea raundi mbili za mwisho.
  Ni moja tu kati ya Medeama na Bejaia inaweza kufikisha pointi 10 iwapo itashinda mechi zote zijazo - maana yake Mazembe imejihakikishai kwenda Nusu fainali kwa pointi zake 10.

  Yanga ya Tanzania inashika mkia kwa pointi yake moja na inasubiri miujiza tu katrika raundi mbili za mwisho ili kwenda Nusu Fainali, baada ya kufunge mechi tatu na kutoa sare moja.
  Mechi zijazo, Yanga itacheza na Mo Bejaia Dar es Salaam na Mazembe itasafiri hadi Ghana kuifuata Medema. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KALABA AIPELEKA MAZEMBE NUSU FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top