• HABARI MPYA

  Friday, July 29, 2016

  TFF YATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI MSIBA WA SENGA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amemtumia salamu za rambirambi Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Theophil Makunga kutokana na kifo cha Joseph Senga – Mpigapicha Mkuu wa Gazeti la Tanzania Daima.
  Rais Malinzi amepokea taarifa za kifo cha mwandishi huyo mwandamizi wa habari aliyebobea kuripoti habari za aina mbalimbali ikiwamo za michezo nchini kilichotokea jioni ya Julai 27, 2016 huko India, alikokuwa akipatiwa matibabu ambako habari za kifo chake zilianza kusambaa usiku wa kuamkia jana Julai 28, 2016 kabla ya kuthibitishwa na Mhariri Mtendaji wa Free Media, Neville Meena.
  Joseph Senga (kushoto) enzi za uhai wake akiwa kazini Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
  Salamu za rambirambi za Rais wa TFF Malinzi pia zimekwenda kwa familia ya marehemu Joseph Senga, ndugu, jamaa na marafiki na kuwataka kuwa na moyo wa subira wakati huu mgumu wa msiba wa mpendwa wao.
  Malinzi alimwelezea Joseph Senga, wakati wa uhai wake alikuwa na mchango mkubwa katika tasnia ya habari za michezo akitoa mawazo yake hivyo ameacha alama ya ucheshi, kujituma na uwajibikaji katika kufanikisha kazi zake katika gazeti la Tanzania Daima na wakati fulani magazeti ya Kampuni ya New Habari House 2006.
  Mwenyezi Mungu aipumzishe roho ya marehemu Joseph Senga mahala pema peponi. Bwana ametoa, Bwana ametwaa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TFF YATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI MSIBA WA SENGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top