• HABARI MPYA

  Sunday, July 31, 2016

  SAMATTA AENDELEZA MOTO WA MABAO GENK, APIGA LA PILI WAKISHINDA 2-1 UBELGIJI

  Na Mwandishi Wetu, GENK
  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta ameendelea kuwa mchezaji muhimu kwa klabu yake, KRC Genk baada ya usiku huu kufunga bao la pili, wakishinda 2-1 dhidi ya KV Oostende.
  Katika mchezo huo wa hatua ya kwanza ya Ligi Kuu ya Ubelgiji, uliofanyika Uwanja wa Luminus Arena mjini Genk, wenyeji walitangulia kwa bao la Nikolaos Karelis dakika ya 50, aliyemalizia pasi ya Sandy Walsh. 

  Nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta akafunga bao la pili dakika ya 90, akimalizia pasi nzuri ya Leandro Trossard kutoka kushoto.
  Samatta (kushoto) akipongezwa na wenzake baada ya kufunga

  Hata hivyo, wakati Genk wameamini wamemaliza mchezo kwa ushindi wa 2-0 baada ya bao la Samatta, KV Oostende wakafanya shambulizi la kushitukiza na mshambuliaji Mzimbabwe, Knowledge Musona akaifungia timu yake bao la kufutia machozi dakika ya tatu ya muda wa nyongeza baada ya kutimia kwa dakika 90 za kawaida.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SAMATTA AENDELEZA MOTO WA MABAO GENK, APIGA LA PILI WAKISHINDA 2-1 UBELGIJI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top