• HABARI MPYA

  Thursday, July 28, 2016

  MSONDO NGOMA WAJA NA‘MSONDO FAMILY DAY’ DDC KARIAKOO JUMAPILI HII

  HATIMAYE lile onyesho kubwa la Msondo Ngoma “Baba ya Muziki” lililopewa jina la ‘Msondo Family Day’, linafanyika Jumapili hii, Julai 31 ndani ya DDC Kariakoo.
  Akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE, mmoja wa maseneta wa Msondo, Abdulfareed Hussein, amesema kuwa onyesho hilo litakuwa na mambo mengi ya kuvutia, ikiwemo zawadi mbali mbali kwa mashabiki wao.
  Abdulfareed amesema kutakuwa na zawadi kwa shabiki atakayependeza, shabiki atakayecheza vizuri staili ya Msondo Ngoma pamoja zawadi kwa shabiki atakayeimba kwa ufasaha wimbo wowote wa Msondo.
  Seneta wa Msondo, Abdulfareed Hussein (kulia) akiwa na gwiji wa bendi hiyo, Shaaban Dede

  Lakini pia kutakuwa na zawadi ya chemsha bongo ya maswali ya papo kwa papo kuhusu mambo mbali mbali yanayohusu Msondo Ngoma ambapo Abdulfareed amefafanua kuwa zawadi zote hizo zitatolewa na maseneta wa Msondo.
  Dhumuni la ‘Msondo Family Day’ ambayo itakuwa inafanyika kila Jumapili ya mwisho wa mwezi, ni kuongeza mshikamano baina ya wanamuziki wa Msondo, mashabiki na wadau wakubwa wa bendi hiyo.
  Ili kuongeza utamu wa onyesho hilo, kundi la Msondo Family litakuwepo ukumbini kulicheza goma la Msondo mwanzo mwisho.
  Tiketi za onyesho hillo litakaloanza saa 12 jioni zinapatikana kwa meneja wa bendi Said Kibiriti ambaye mawasiliano yake ya simu ni 0655 921 223 na kwa wale ambao hawataweza kununua tiketi mapema, basi zitapatikana mlangoni siku ya onyesho kwa buku 10 tu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MSONDO NGOMA WAJA NA‘MSONDO FAMILY DAY’ DDC KARIAKOO JUMAPILI HII Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top