• HABARI MPYA

    Tuesday, February 03, 2026

    MBEYA CITY YALAZIMISHWA SARE NA DODOMA JIJI 1-1 SOKOINE


    WENYEJI, Mbeya City wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Dodoma Jiji FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara mchana wa leo Uwanja Wa Sokoine Jijini Mbeya.
    Ni wageni waliotangulia kwa bao la mshambuliaji wao hatari, William Edgar dakika ya 10, kabla ya mshambuliaji mwingine, Eliud Ambokile kuisawazishia Mbeya City dakika ya 26.
    Kwa matokeo hayo, Mbeya City inafikisha pointi 10 katika mchezo wa 13 na kupanda kwa nafasi moja hadi ya 13 katika ligi ya tiny 16, wakati Dodoma Jiji inafikisha pointi 14 katika mchezo wa 13 na kupanda kwa nafasi moja pia hadi ya nane. 
    Next
    This is the most recent post.
    Older Post
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MBEYA CITY YALAZIMISHWA SARE NA DODOMA JIJI 1-1 SOKOINE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top