• HABARI MPYA

    Wednesday, July 27, 2016

    AZAM FC YALETA MSHAMBULIAJI MZIMBABWE 'NGOMA ANASUBIRI'

    Na Mwandishi Wetu, ZANZIBAR
    NYOTA wa timu ya Caps United ya Zimbabwe, Brian Abbas Amidu ambaye anasifiwa ni hatari kulio Donald Ngoma wa Yanga, ametua visiwani Zanzibar leo mchana tayari kuanza majaribio ya kujiunga na mabingwa wa Afrika Mashariki na Kati, Azam FC.
    Amidu aliyetua nchini jana akitokea Zimbabwe, mara baada ya kutua visiwani hapa alianza moja kwa moja mazoezi na wenzake wakati wakifanya programu maalumu ya kunyoosha viungo kwenye bwawa la kuogelea ndani ya Hoteli ya Kitalii ya Mtoni Marine ilipofikia Azam FC.
    Brian Abbas Amidu (kulia) akipeana mkono na Kocha Mkuu wa Azam FC, Zebensul Hernandez Rodriguez (kushoto). Katikati ni Ofsa Habari, Jaffar Iddi Maganga

    Mshambuliaji huyo, 26, mwenye uwezo pia wa kucheza kama kiungo mshambuliaji hakuwa na maneno mengi ya kusema mara baada ya kuwasili bali ameweka wazi kuwa yupo tayari kupambana na kuonyesha kipaji chake ili hatimaye aweze kufuzu na kusajiliwa.
    Amidu anaungana na nyota mwingine wa Kimataifa wa Zimbabwe, Bruce Kangwa, ambaye bado anaendelea na majaribio yake akiwa ametimiza wiki moja hivi leo.
    Mbali na kucheza katika kikosi cha Caps United, Amidu amefanikiwa kucheza soka la kulipwa kwa miaka minne kabla ya Januari mwaka huu kurejea nyumbani na kujiunga na Caps.
    Usajili wake wa kwanza kucheza kimataifa ilikuwa ni mwaka 2012 alipojiunga na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini kasha akapelekwa Black Leopards ya huko kabla ya Machi mwaka jana kutua Masafi SC inayoshiriki Ligi Kuu ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).
    Wachezaji wengine waliokuwa kwenye majaribio Azam FC ni washambuliaji Ibrahima Fofana (Ivory Coast) anayeweza pia kucheza kama winga wa kushoto pamoja na Mrundi Fuadi Ndayisenga.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM FC YALETA MSHAMBULIAJI MZIMBABWE 'NGOMA ANASUBIRI' Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top