• HABARI MPYA

  Tuesday, July 26, 2016

  SHEIKH SAID BADO MAKAMU MWENYEKITI TPLB

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  ALHAJ  Sheikh Said Mohamed bado ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) baada ya kuingia kwenye wadhifa huo katika uchaguzi uliofanyika Oktoba 2013.
  Nafasi hiyo ya Mohamed ni kwa mujibu wa Kanuni za Uendeshaji za TPLB, na aliipata kupitia uchaguzi huo. Pia Makamu Mwenyekiti huyo ni Mwenyekiti wa klabu ya Azam FC inayoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom.
  Mohamed alikuwa Meneja Mkuu wa Kampuni ya Salim Said Bakhresa ambayo pia inamiliki pia timu ya Azam FC kabla ya kustaafu Mei mwaka huu. Licha ya kustaafu ajira yake ndani ya SSB, lakini Bw. Mohamed bado ni Mwenyekiti wa Azam FC.
  Sheikh Said Mohammed bado Makamu Mwenyekiti wa TPLB

  Kwa mujibu wa Katiba ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa TPLB pia ni wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho hilo na wanaendelea na majukumu yao kama kawaida.
  Uchaguzi ujao wa viongozi wa TPLB ambayo inaongozwa na Mwenyekiti wake Hamad Yahya unatarajiwa kufanyika mwakani.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SHEIKH SAID BADO MAKAMU MWENYEKITI TPLB Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top