• HABARI MPYA

    Friday, July 22, 2016

    SAM ALLARDYCE NDIYE KOCHA MPYA TIMU YA TAIFA YA ENGLAND

    Sam Allardyce ametangazwa rasmi kuwa kocha mpya wa England PICHA ZAIDI GONGA HAPA 

    HISTORIA YA UKOCHA YA SAM ALLARDYCE

    1991-92: Limerick (kocha-mchezaji)
    1994-96: Blackpool
    1997-99: Notts County
    1999-2007: Bolton Wanderers
    2007-08: Newcastle United
    2008-2010: Blackburn Rovers
    2011-15: West Ham United
    2015-16: Sunderland 
    CHAMA cha Soka (FA) England kimemthibitisha Sam Allardyce kuwa kocha moya wa timu ya taifa, baada ya kuondoka Sunderland. 
    Anakuwa kocha wa 14 wa England akichukua nafasi ya Roy Hodgson, ambaye alijiuzulu baada ya matokeo mabaya kwenye michuano ya Euro 2016 wakitolewa na Iceland. 
    Kocha huyo mwenye uzoefu na Ligi Kuu ya England amesaini Mkataba wa miaka miwili na ataanza kuiongoza Three Lions katika mechi za kufuzu Kombe la Dunia mwaka 2018 mwezi Septemba. Allardyce amewataka wachezaji wake wapya atakaowaita kuifanya nchi ijivunie tena. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SAM ALLARDYCE NDIYE KOCHA MPYA TIMU YA TAIFA YA ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top