• HABARI MPYA

    Friday, July 29, 2016

    KIMEELEWEKA, JUVENTUS YAKUBALI KUMRUDISHA POGBA MAN UNITED

    KIUNGO wa kimataifa wa Ufaransa, Paul Pogba atakuwa mchezaji wa Manchester United tena baada ya kufikia makubaliano ya dili la uhamisho wa Pauni Milioni 100 na Juventus usiku wa Alhamisi.
    Inamaanisha mchezaji huyo aliyeondoka Old Trafford bure mwaka 2012 atarejea kama mchezaji babu kubwa - aliyesajiliwa kwa dau la rekodi duniani.
    Dili la nyota huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 23 linatarajiwa kukamilishwa Ijumaa baada ya wakala wa Pogba, Mino Raiola kuwa na mazungumzo ya kina na viongozi wa Juventus na wanasheria mjini Turin mchana wa Alhamisi. 
    United na Juventus zzimekubaliana kumlipa Raiola sehemu ya asilimia yake 20 katika mauziano ya Pogba.

    Paul Pogba atakuwa analipwa mshahara wa Pauni 290,000 kwa wiki Man United  PICHA ZAIDI GONGA HAPA 


    TAKWIMU ZA POGBA MSIMU WA 2015-2016 

    Mechi alizocheza: 42
    Mabao aliyofunga: 10
    Pasi za mabao: 12
    Dakika alizopcheza: 3621
    Pogba anatarajiwa kufanyiwa vipimo mjini Los Angeles, Marekani alitangulia kwa mapumziko mjini Florida.
    Na amekubali kusaini mkataba wa miaka mitano, ambao utamfanya alipwe mshahara wa Puni 290,000 kwa wiki. 
    Pogba aliondoka Old Trafford Julai mwaka 2012 baada ya kocha wa Man United wakati huo, Sir Alex Ferguson kukataa ombi la Raiola kuuboresha kidogo mkataba. Juventus ililipa Pauni 800,000 kumpata.
    Atakuwa mchezaji wa nne kusajiliwa na kocha mpya, Mreno Jose Mourinho baada ya beki Eric Bailly, mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic na kiungo mshambuliaji Henrikh Mkhitaryan.
    Muargentina Angel Di Maria alikuwa mchezaji ghali wa mwisho kusajiliwa England, akinunuliwa kwa Pauni Milioni 59.7 na Man United kutoka Real Madrid Agosti mwakaa 2014.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KIMEELEWEKA, JUVENTUS YAKUBALI KUMRUDISHA POGBA MAN UNITED Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top