• HABARI MPYA

  Friday, July 29, 2016

  AKINA SAMATTA WAPATA USHINDI MWEMBAMBA NYUMBANI EUROPA LEAGUE

  Na Mwandishi Wetu, GENK
  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta ‘Sama Goal’ usiku wa Alhamisi ameiongoza timu yake, KRC Geenk kupata ushindi mwembamba wa 1-0 dhidi ya Cork City FC ya Ireland katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Tatu ya mchujo wa kuwania kuingia hatua ya makundi ya michuano ya Europa League.
  Baada ya matokeo hayo Uwanja wa Luminus Arena, KRC Genk sasa watatakiwa kulazimisha sare katika mchezo wa marudianio Agosti 4 nchini Ireland ili kusonga mbele. 
  Samatta alicheza kwa dakika zote 90, lakini bao pekee la KRC Genk lilifungwa na Mjamaica, Leon Bailey dakika ya 31.
  Genk ilifika hatua hii baada ya kuitoa Buducnost ya Montenegro kwa penalti 4-2 Uwanja wa Pod Goricom mjini Podgorica katika mchezo wa marudiano Raundi ya Pili ya mchujo, Genk ikianza kushinda 2-0, mabao ya Neeskens Kebano kwa penalti dakika ya 16 na Samatta dakika ya 79 Alhamisi wiki iliyopita kabla ya Buducnost kulipa kisasi kwa ushindi wa 2-0, mabao ya Radomir Dalovic dakika ya kwanza na Milos Raickovic dakika ya 39.
  Kikosi cha KRC Genk kilikuwa: Bizot, Walsh, Dewaest Wouters, Uronen, Ndidi, Pozuelo/Heynen dk82, Bailey, Buffalo, Karelis/Kebano dk71 na Samatta.
  Cork City FC : McNulty, Bennett, Bolger, Beattie/Daniel Morrissey dk82, Dooley, O'Connor, Morrissey, McSweeney, Browne, Maguire/O'Sullivan dk85 na Buckley.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AKINA SAMATTA WAPATA USHINDI MWEMBAMBA NYUMBANI EUROPA LEAGUE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top