• HABARI MPYA

  Thursday, July 07, 2016

  NYAGAWA AREJESHWA SIMBA, ABBAS ‘ASTAAFISHWA’

  Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
  SIMBA SC immrejesha Nahodha wake wa zamani, Nico Nyagawa kuwa Meneja wa timu, akichukua nafasi ya Abbas Ally ambaye anaondolewa.
  Msimu uliopita Simba SC ilifanya mabadiliko ya benchi la Ufundi na Nyagawa akaondolewa nafasi yake ikichukuliwa na Abbas.

  Nico Nyagawa (kulia) amerejeshwa kuwa Meneja wa Simba, akichukua nafasi ya Abbas Ally ambaye aliyeondolewa

  Na kuelekea msimu mpya, uongozi wa Simba umeamua kumrejesha kiungo wake wa zamani, Nico Nyagawa baada ya kugundua mapungufu makubwa juu ya Abbas.
  Na kikubwa kinachomuondoa Abbas Simba SC ni kushindwa kuwa kiunganishi kizuri kati ya makocha na wachezaji na wakati mwingine kujiruhusu yeye mwenyewe kuingia kwenye ugomvi na wachezaji.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NYAGAWA AREJESHWA SIMBA, ABBAS ‘ASTAAFISHWA’ Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top