TIMU ya KMC FC imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mashujaa FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara usiku hui Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi.
Bao pekee la KMC FC limefungwa na mshambuliaji Daruweshi Saliboko dakika ya 22 na kwa ushindi huo wanafikisha pointi nane katika mchezo Wa 13, ingawa wanaendelea kushika mkia kwenye ligi ya timu 16.
Kwa upande wao Mashujaa baada ya kupoteza mchezo huo wanabaki na pointi zao 13 za mechi 12 nafasi ya 10.




.png)
0 comments:
Post a Comment