• HABARI MPYA

  Friday, July 01, 2016

  ETOILE DU SAHEL YALAZIMISHWA SARE NYUMBANI KOMBE LA SHIRIKISHO

  TIMU ya Etoile Sahel ya Tunisia imelazimishwa sare ya 1-1 nyumbani usiku wa jana na FUS Rabat ya Morocco katika mchezo wa Kundi B Kombe la Shirikisho Afrika.
  Ahmed Akaichi alianza kuwafungia wenyeji dakika ya tatu katika mji wa bahari ya Mediterranean, Sousse, kabla ya Abdessalam Benjelloun kuwasawazishia wageni katikati ya kipindi cha pili Uwanja wa Olimpiki.
  Kawkab Marrakech sasa inaongoza kundi hilo baada ya Jumapili kushinda ugenini 2-1 dhidi ya Al Ahly Tripoli ya Libya, wakati FUS inafuatia kwa pointi zake nne, na Etoile ina pointi moja sawa na Ahly.
  Etoile Sahel ya Tunisia imelazimishwa sare ya 1-1 nyumbani usiku wa jana na FUS Rabat ya Morocco

  Katika Kundi A, TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) inaongoza kwa pointi zake sita pi, ikifuatia na Mouloudia Bejaia ya Algeria yenye pointi nne, Medeama ya Ghana pointi moja na Yanga ya Tanzania inashika mkia haina pointi.
  Mechi za kukamilisha mzunguko wa kwanza wa makundi hiyo yenye hadhi sawa na Europa League ya UEFA zitachezwa katikati ya Julai.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ETOILE DU SAHEL YALAZIMISHWA SARE NYUMBANI KOMBE LA SHIRIKISHO Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top