• HABARI MPYA

    Friday, July 01, 2016

    WYDAD, MAMELODI ZAONGOZA MAKUNDI LIGI YA MABINGWA AFRIKA

    TIMU za Wydad Casablanca ya Morocco na Mamelodi Sundowns zinaongoza maakundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya mechi za katikati ya wiki hii.
    Wydad Casablanca iliifunga 2-0 Zesco United juzi mjini Casablanca na kufikisha pointi sita katika Kundi A, mbele ya ASEC Mimosa iliyoshinda 2-1 ugenini dhidi ya Al Ahly mjini Cairo Misri na kupata pointi tatu za kwanza, wakati Zesco pia ina pointi tatu na Al Ahly haina pointi inashika mkia. 
    Mamelodi Sundowns ilishinda 2-1 nyumbani dhidi ya Enyimba ya Nigeria Jumanne na kupata pointi tatu za kwanza hivyo kuongoza Kundi B kwa wastani wa mabao, ikilingana pointi na Zamalek ya Misri ambayo haikuwa na mechi baada ya CAF kuiondoa ES Setif ya Algeria mashindanoni kwa vurugu za mashabiki wake.
    Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini inaongoza Kundi B Ligi ya Mabingwa Afrika
    Enyimba inashika mkia katika kundi hilo ikiwa haina pointi baada ya kucheza mechi, tofauti na wapinzani wake, Mamelodi na Zamalek ambazo kila moja imecheza mechi moja.
    ES Setif iliondolewa kufuatia vurugu kubwa zilizofanywa na mashabiki wake katika mchezo dhidi ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini Juni 19 iliyopita.
    Ripoti ya marefa ilisema amani ilichafuka uwanjani baada ya mashabiki kurusha mioto, chupa na mawe na kusababisha watu kadhaa kujeruhiwa kabla ya walinzi kuingilia kati kutuliza hali hiyo. 

    Kundi A

    NaTimuPWDLGFGAGDPts
    1Wydad Casablanca22003036
    2ASEC Mimosas21012203
    3Zesco United210134-13
    4Al Ahly200235-20

    Kundi B

    NaTimuPWDLGFGAGDPts
    1Mamelodi Sundowns11002113
    2Zamalek11001013
    3Enyimba200213-20
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: WYDAD, MAMELODI ZAONGOZA MAKUNDI LIGI YA MABINGWA AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top