• HABARI MPYA

  Sunday, July 10, 2016

  CAF WAILIMA FAINI YA ‘MADOLA YA KIMAREKANI’ YANGA

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  SHIRIKISHO la Soka Afrika limeitoza faini ya dola za Kimarekani 10,000 klabu ya Yanga baada ya wachezaji wake kumzonga refa katika mchezo dhidi ya Sagrada Esperanca nchini Angola Mei 18, mwaka huu.
  Hatua hiyo imechukuliwa katika kikao cha Bodi ya Nidhamu ya CAF kilichofanyika Julai 3, mwaka huu mjini Cairo, Misri.
  Katika mchezo huo wa marudiano wa mchujo wa kuwania kufuzu hatua ya makundi Kombe la Shirikisho, ambao wenyeji walishinda 1-0, Yanga ilifuzu kwa ushindi wa jumla wa 2-1 baada ya awali kushinda 2-0 Dar es Salaam.
  Na taarifa ya CAF kwa BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE leo imesema kwamba katika mchezo huo namba 100 wa Kombe la Shirikisho, wachezaji wa Yanga walimzonga refa na kusababisha mechi kusimama kwa muda.
  Na kwa kosa hilo, Yanga wanatakiwa kulipa dola 5,000 (zaidi ya Sh. Milioni 10) katika faini ya dola 10,000 (zaidi ya Sh. Milioni 20) na 5,000 nyingine watazilipa kama ziada ya adhabu nyingine iwapo watarudia kosa.    
  Wapinzani wa Yanga katika Kundi A, MO Bejaia pia wametozwa faini ya dola 10,000 baada ya mashabiki wake kufanya vurugu katika mechi dhidi ya mabingwa wa Tanzania Juni 18 nchini Algeria.
  Taarifa hii inamaanisha Yanga imenusurika adhabu yoyote baada ya mechi zake mbili za awali za Kundi A, wakifungwa 1-0 na MO Bejaia na 1-0 pia na TP Mazembe Dar es Salaam, mchezo ambao mashabiki waliingia bure.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CAF WAILIMA FAINI YA ‘MADOLA YA KIMAREKANI’ YANGA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top