• HABARI MPYA

    Sunday, July 10, 2016

    MALINZI AWAPA POLE WAANDISHI WA HABARI KWA MSIBA WA MWENZAO

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amemtumia salamu za rambirambi Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), Juma Pinto kufuatia kifo cha Elizabeth Mayemba (pichani kulia)- Mwandishi wa Habari za Michezo wa Gazeti la Majira.
    Rais Malinzi amesema, amepokea taarifa za kifo cha mwandishi huyo mwandamizi wa habari za michezo nchini kilichotokea Julai 09, 2016 na habari zake kuanza kusambaa majira ya jioni jana kabla ya kuthibitishwa na wanafamilia na uongozi wa TASWA kupitia njia mbalimbali za mawasiliano.
    Salamu za rambirambi za Rais wa TFF Malinzi pia zimekwenda kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa na marafiki na kuwataka kuwa na moyo wa subira wakati huu mgumu wa msiba wa Elizabeth Mayemba.
    Elizabeth Mayemba, wakati wa uhai wake alikuwa na mchango mkubwa katika tasnia ya habari za michezo akitoa mawazo yake hivyo ameacha alama ya ucheshi, kujituma na uwajibikaji katika kufanikisha kazi zake katika gazeti la Majira na wakati fulani magazeti ya Kampuni ya New Habari House 2006.
    Mwenyezi Mungu aipumzishe roho ya marehemu Elizabeth Mayemba mahala pema peponi. Amin.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MALINZI AWAPA POLE WAANDISHI WA HABARI KWA MSIBA WA MWENZAO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top