KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger ameamua kubaki katika klabu hiyo baada ya kuiongoza Gunners kumaliza ukame wa miaka tisa wa mataji kufuatia kuilaza Hull City mabao 3-2 na kutwaa Kombe la FA usiku huu Uwanja wa Wembley.
Hull iliwavunja nguvu mashabiki wa Gunners kwa mabao mawili ya haraka ya kuongoza ndani ya dakika nane, lakini timu ya Wenger ikazinduka na kusawazisha yote kabla ya Aaron Ramsey kufunga la kuongeza ndani ya dakika 30 za nyongeza.
Wenger amesema kwamba matokeo hayo ya Wembley hapaa shaka yanamfanya ajisikie faraja kubakia Emirates na amethibitisha haondoki.
"Wakati wore nimesema mustakabali wangu hautegemei hili, lakini wakati wore nimesema nilitaka kubaki," alisema Wenger alipoulizwa na ITV kama atabaki, kabla ya kusema , "Ndiyo, nitabaki.'
"Tulitaka kuweka historia usiku huu na kushinda mechi na tumefanya hivyo, hizo ni namna zote - namna ya kuianza fainali ya Kombe na namna ya kuzinduka," alisema Wenger.
Furaha tupu: Wenger akiinua Kombe la FA kusherehekea na wachezaji wake
Mshindi wa mechi: Aaron Ramsey alifunga bao la ushindi na hapa anasherehekea na Kombe la FA
0 comments:
Post a Comment