SHIRIKISHO la Soka Nigeria (NFF) limetangaza kikosi cha cha awali
cha wachezaji 30 kwa ajili ya Fainali za Kombe la Dunia la FIFA nchini Brazil
baadaye mwaka huu.
Kutangazwa kwa wachezaji hao jana, kumefutia kikao cha pamoja
baina ya NFF na kocha wa Super Eagles, Stephen Keshi.
Kikosi hicho ni makipa; Vincent Enyeama, Austin Ejide, Chigozie
Agbim na Daniel Akpeyi; Mabeki: Elderson Echiejile, Juwon Oshaniwa, Godfrey
Oboabona, Azubuike Egwuekwe, Kenneth Omeruo, Joseph Yobo, Kunle Odunlami na Efe
Ambrose.
Viungo:
John Mikel Obi, Ogenyi Onazi, Ramon Azeez, Joel Obi, Nosa Igiebor, Michael
Uchebo, Ejike Uzoenyi, Sunday Mba na Reuben Gabriel, wakati washambuliaji ni:
Ahmed Musa, Shola Ameobi, Emmanuel Emenike, Obinna Nsofor, Osaze Odemwingie,
Babatunde Michael, Victor Moses, Uche Nwofor na Nnamdi Oduamadi.
![]() |
Kocha wa Nigeria, Stephen Kheshi ametaja kikosi cha wachezaji 30 cha awali kwa ajili ya Kombe la Dunia |
Nigeria ni moja kati ya nchi tano za Afrika zitakazoshiriki fainali za Kombe la dunia mwaka huu, pamoja na Algeria, Ghana na Ivory Coast.
0 comments:
Post a Comment