• HABARI MPYA

    Thursday, July 21, 2016

    YANGA KUONDOKA JUMAMOSI KUWAFUATA MEDEAMA WAKAWAPIGIE HUKO HUKO KWAO

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    MSAFARA wa watu 30 wa Yanga SC, wakiwemo wachezaji 20 unatarajiwa kuondoka Jumamosi kwenda Ghana tayari kwa mchezo wa marudiano Kundi A Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya wenyeji Medeama wiki ijayo. 
    Yanga iliingia kambini leo katika hoteli ya Tiffany, katikati ya jiji la Dar es Salaam kuanza rasmi maandalizi ya mchezo huo huki ikifanya mazoezi Uwanja wa Chuo cha Polisi, Kurasini.
    Yanga watakuwa wageni wa Medeama Jumatano ya Julai 27, mwaka huu Uwanja wa Sekondi Sports au Essipong mjini Sekondi-Takoradi, Ghana.
    Makocha wa Yanga, Mholanzi Hans van der Pluijm (kulia) na mzawa Juma Mwambusi (kushoto)
    Siku hiyo, vinara wa kundi hilo, TP Mazembe wataikaribisha Mouloudia Olympique Bejaia mjini Lubumbashi.
    Timu hizo zitarudiana kiasi cha wiki baada ya kutoa sare katika mechi zao za kwanza, Yanhga 1-1 na Medema ana MO Bejaia 0-0 na Mazembe.
    Mazembe inaongoza Kundi A kwa pointi zake saba, ikifuatiwa na MO Bejaia pointi tano, Medeama pointi mbili, wakati Yanga yenye pointi moja inashika mkia.  
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA KUONDOKA JUMAMOSI KUWAFUATA MEDEAMA WAKAWAPIGIE HUKO HUKO KWAO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top