• HABARI MPYA

    Thursday, July 21, 2016

    TOTAL WADHAMINI WAKUU WAPYA MICHUANO YA AFRIKA

    Na Mwandishi Wetu, PARIS
    KAMPUNI ya Total imeingia Mkataba na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kuwa mdhamini Mkuu wa mashindano yote yanayoandaliwa na bosi hiyo ya kandanda barani kwa miaka nane ijayo.
    Total itaanza kudhamini mashindano ya CAF kwenye Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON), kuanzia Januari 14 hadi Februari 5 mwakani nchini Gabon, yakibadilishwa jina na kuwa Total AFCON 2017.
    Rais wa CAF, Issa Hayatou amesema kwamba udhamini huo wa Total ni hatua nzuri ya maendeleo kwao katika mikakati yao ya kuiinua zaidi soka ya Afrika.
    Kwa upande wake, Rais na Mtendaji Mkuu wa Total, Patrick Pouyanne, amesema wamefurahi kufunga ndoa na CAF na watajitahidi kuhakikisha wanasaidia kuinua zaidi soka ya Afrika.
    Pamoja na AFCON, Total watakuwa wadhamini wa Michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN), inayoshirikisha wachezaji wanaocheza ligi za nchini mwao pekee, michuano ya klabu, yaani Ligi ya Mabingwa, Kombe la Shirikisho na Super Cup, michuano ya kuanzia U-23, U-20 na U-17, michuano ya wanawake na Futsal.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TOTAL WADHAMINI WAKUU WAPYA MICHUANO YA AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top