• HABARI MPYA

  Thursday, July 21, 2016

  MARIO GOTZE AREJEA BORUSSIA DORTMUND BAADA YA 'KUTEMWA' BAYERN MUNICH

  Borussia Dortmund imethibitisha kumrejesha kiungo Mario Gotze kutoka Bayern Munich  PICHA ZAIDI GONGA HAPA  

  WASOFU WA MARIO GOTZE:  

  Umri: Miaka 24
  Nafasi: Kiungo mshambuliaji
  Klabu: Borussia Dortmund (2009-2013), 
  Bayern Munich (2013-2016), 
  Borussia Dortmund (Tangu 2016t)
  Mataji aliyoshinda: Matano
  Bundesliga matatu, Kombe la Ujerumani matatu, Kombe la Dunia la Klabu moja, Kombe la Dunia moja akiwa na Ujerumani
  Mechi za Kimataifa: 56, mabao 17  
  KLABU ya Borussia Dortmund imethibitisha kumsajili tena kiungo Mario Gotze kutoka kwa mahasimu wao wa Bundesliga, Bayern Munich kwa dau la Pauni Milioni 22.
  Dortmund imetangaza usajili kupitia tovuti yao ikisema kwamba Gotze - aliyejiunga na Bayern Munich mwaka 2013 akwa dau la Pauni Milioni 32 - amekubali kusaini Mkataba wa hadi mwaka 2020 na atakamilisha uhamisho wake baada ya vipimo vya afya.
  Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 alikuwa amebakiza mwaka mmoja katika Mkataba wake na mabingwa wa Bundesliga, lakini anaondoka Bayern baada ya kuambiwa hatakuwamo kwenye mipango ya kocha mpya, Carlo Ancelotti msimu ujao Allianz Arena.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MARIO GOTZE AREJEA BORUSSIA DORTMUND BAADA YA 'KUTEMWA' BAYERN MUNICH Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top