• HABARI MPYA

  Sunday, July 03, 2016

  UJERUMANI YAWANG'OA KWA MATUTA ITALIA EURO 2016

  Wachezaji wa Ujerumani wakifurahi baada ya kuitoa kwa penalti 6-5 Italia kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 120 katika mchezo wa Robo Fainali Euro 2016 usiku huu Uwanja wa Stade Matmut-Atlantique mjini Bordeaux, Ufaransa. Ujerumani ilitangulia kwa bao la Mestu Ozil dakika ya 65, kabla ya Leonardo Bonucci kuisawazishia Italia dakika ya 78 kwa penalti baada ya beki Jerome Boateng kuunawa mpira katika eneo la hatari.
  Waliofunga penalti za Ujerumani ni Toni Kroos, J. Draxler, M. Hummels, J. Kimmich, J. Boateng na J. Hector, wakati T. Müller, M. Özil na B. Schweinsteiger walikosa. Waliofunga penalti za Itali ni L. Insigne,  A. Barzagli,  E. Giaccherini, M. Parolo na  M. De Sciglio, wakati waliokosa ni S. Zaza, G. Pellè,  L. Bonucci na  M. Darmian PICHA ZAIDI GONGA HAPA 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: UJERUMANI YAWANG'OA KWA MATUTA ITALIA EURO 2016 Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top