TIMU ya Azam FC imeweka hai matumaini ya kwenda Robo Fainali Kombe la Shirikisho Afrika baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Nairobi United ya Kenya katika mchezo wa Kundi B usiku huu Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.
Bao pekee la Azam FC leo limefungwa na kiungo wake nyota, Feisal Salum Abdallah ‘Fei Toto’ dakika ya 12 na kwa ushindi huo, Azam FC wanafikisha pointi sita ingawa wanabaki nafasi ya tatu nyuma ya Wydad Athletics ya Morocco na AS Maniema Union ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), zenye pointi tisa kila moja, wakati Nairobi United inaendelea kushika mkia kufuatia kufungwa mechi zake zote nne.
Mechi zijazo Azam FC watawakaribisha AS Maniema Union hapo hapo Zanzibar na Nairobi United watakuwa wenyeji wa Wydad AC Uwanja wa Taifa wa Nyayo, Nairobi mechi zote zikichezwa Februari 8, mwaka huu.



.png)
0 comments:
Post a Comment