• HABARI MPYA

    Sunday, July 03, 2016

    SIMBA YASHUSHA STRAIKA WA IVORY COAST

    Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
    SIMBA SC imemaua – baada ya kuingia Mkataba na kocha Mcameroon Joseph Marius Omog sasa imehamia kwenye kusajili wachezaji bora wa kigeni.
    Wakati tayari ikiwa imefikia makubaliano na mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi, Laudit Mavugo aje kusiani Mkataba wa miaka miwili, Simba SC inaleta mshambuliaji hatari kutoka Ivory Coast.
    Huyo ni Goue Frederic Noel Blagnon aliyezaliwa Desemba 26, mwaka 1985 ambaye anatokea klabu ya African Sports ya kwao, Ivory Coast.
    Goue Frederic Noel Blagnon akimiliki mpira ya wachezaji wa timu pinzani wakati anacheza Asante Kotoko ya Ghana

    Mchezaji huyo wa zamani wa Union Sportive de Bitam ya Gabon na Asante Kotoko ya Ghana, anakuja Simba SC kwa msaada wa kipa Muivory Coast wa timu hiyo, Vincent Angban.
    Blagnon anayependa kuvaa jezi namba 11, anatarajiwa kuwasili usiku huu pamoja na kipa Angban na Jumatatu anaweza kuwa mazoezi Simba SC, ili kwanza kocha Omog amuone na kujiridhisha juu ya uwezo wake.   
    Omog alisaini Mkataba wa miaka miwili Ijumaa, ikiwa ni siku moja baada ya kuwasili nchini na anarithi mikoba ya
    Goue Blagnon anakuja Simba
    Muingereza Dylan Kerr aliyetimuliwa mapema mwaka huu na nafasi yake kukaimishwa Mganda Jackson Mayanja.

    Ingawa Simba SC inataka Mayanja aendelee na kazi kama Msaidizi wa Omog, lakini hakuna uhakika kama hilo litawezekana na tayari taarifa zisizo rasmi zinasema Mganda huyo anataka kurejea Kagera Sugar.
    Simba SC inatarajiwa kuanza mazoezi Jumatatu na wachezaji kadhaa wapya wanatarajiwa kuhudhuria ili kufanyiwa majaribio.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA YASHUSHA STRAIKA WA IVORY COAST Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top