• HABARI MPYA

  Monday, July 04, 2016

  TANZANIA YAPEWA IVORY COAST KUFUZU FAINALI ZA AFRIKA UFUKWENI 2016

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  TANZANIA itacheza na Ivory Coast kuwania kufuzu kwenye fainali za Soka ya Ufukweni nchini Nigeria baadaye mwaka huu. 
  Taarifa ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kwa BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE imesema kwamba mchezo wa kwanza utafanyika Abidjan kati ya Agosti 26, 27 na marudiano yatafanyika Dar es Salaam kati ya Septemba 16, 17 na 18, mwaka huu.
  Timu nyingine zilizomo kwenye kinyang’anyiro hicho mbali ya Tanzania na Ivory Coast ni Cape Verde, Ghana, Misri, Liberia, Libya, Kenya, Madagascar, Morocco, Msumbiji, Senegal, Sudan na Uganda.
  Mchezaji wa Tanzania (kushoto) akimtoka mchezaji wa Misri Machi 14, mwaka jana katika ufukwe wa Escape One, Mikocheni, Dar es Salaam. Tanzania ilifungwa 6-2
  Kutakuwa ne mechi moja moja tu za kuwania kufuzu ambapo washindi saba wataungana na wenyeji Nigeria kwenye fainali hizo zinazotarajiwa kuanza Desemba 13 hadi 18, mwaka huu.
  Timu zitakazoingia fainali ya michuano hiyo, zitaiwakilsha Afrika kwenye Kombe la Dunia la FIFA la Soka ya Ufukweni ambalo fainali zake zitafanyika Bahamas kuanzia Aprili 27 hadi Mei 7 mwaka 2017.
  Madagascar ndiyo walikuwa mabingwa wa mwaka 2015 baada ya kuifunga Senegal kwa penalti 2-1 kwenye fainali nchini Shelisheli.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TANZANIA YAPEWA IVORY COAST KUFUZU FAINALI ZA AFRIKA UFUKWENI 2016 Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top