• HABARI MPYA

    Monday, July 04, 2016

    SMALLING AANGUKIA KICHWA NA KUUMIA BAADA YA KULISHWA SUMU KWENYE CHAKULA

    BEKI wa Manchester United, Chris Smalling ameshonwa nyuzi tatu juu ya jicho lake la kulia baada ya kuumia akiwa mapumzikoni mjini Bali.
    Majanga hayo yamemkuta beki huyo tegemeo wa Mashetani Wekundu akiwa mapumzikoni na mpenzi wake, Sam Cooke kisiwa hicho cha Indonesia na kukimbizwa hospitali.
    Taarifa ya United imesema Smalling alipoteza fahamu na kuangukia kichwa, baada ya kula chakula chenye sumu na picha zinamuonyesha mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 akiwa amefungwa bandeji kichwani, shingoni na mkono wa kushoto.
    Chris Smalling akipatiwa matibabu kisiwa cha Bali nchini Indonesia baada ya kuumia  

    Tayari Smalling ameruhusiwa na Madaktari kuondoka hospitali na amerejea kuendelea na mapumziko yake na atawasili Carrington baadaye mwezi huu kama ilivyopangwa.
    Yupo kwenye mapumziko ya wiki tatu baada ya England kutolewa Euro 2016 Ufaransa na anatarajiwa kuungana na kikois cha Jose Mourinho kwa ziara ya China kujiandaa na msimu mpya. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SMALLING AANGUKIA KICHWA NA KUUMIA BAADA YA KULISHWA SUMU KWENYE CHAKULA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top